Wednesday, February 4, 2009

KINGA

Mada ya leo ni nzito na nyeti. Jaribu kuisoma bila kuzingatia itikadi ama imani yako. Falsafa ya "Jielimishe kama vile utaishi daima" inafaa hapa. Natumaini maelezo haya kuhusu condom kama kinga yatakua na faida kwa wanaume wengi na wanawake watakaosoma.

Mada yangu haitahusu moja kwa moja elimu juu ya matumizi sahihi ya kondomu. Ingia hapa kwa maelezo sahihi: http://www.information-condom-source.com/
Ninachotaka kugusia hapa ni tatizo la wanaume wengi kutoipenda kondomu na hivyo kutoitumia.

Katika mazungumzo yetu huwa tunatania kuhusu ujinga wa " kula pipi na ganda lake" Utamu wa pipi ni mate hivyo pipi inatakiwa kuliwa baada ya kutupa ganda. Ni kweli, lakini "pipi" siku hizi imeingiwa nuksi.

Sisi wanaume tunaweza kuwa karibu sana lakini tabia zetu katika tendo la ngono ni siri zetu. Inawezekana washkaji wawili wakaopoa loose sehemu, wakaenda wakapiga kila mmoja chumbani kwake au chumba kimoja lakini swala la "oya, unatumia zana!" lisizungumzwe.

Mwanaume hapendi kitu chochote ambacho kinampa changamoto dhidi ya nafsi yake. Kondomu ni moja ya zana muhimu kujilinda dhidi ya magonjwa ya zinaa na kuzuia mimba, lakini wanaume wengi wanagwaya kuzitumia kwa sababu mbalimbali:

- Kuu ni kwamba zinapunguza sana ladha ya tendo la ndoa!

- Zinaweza kukawiza kishindo (nzuri na mbaya kwani mchezo wenyewe ni mzuri pande zote mbili zikicheza sawia)

- Zinakata mstimu kabla ya tendo. Hili ndio haswa tonge la moto katika tendo. Mwanaume hapendi jogoo kugoma kuwika!

- Zinabana/zinapwaya

- Zinawasha

- Zinanukia vibaya

- Waanume wanaona noma kununua kondomu nk.













Of course condom zinaumbua wale ambao wameoa au wanamahusiano "rasmi" na wapenzi wao. Ikiwa kwenda kununua ni tabu, swala la kuzihifadhi linaleta utata zaidi!

Lakini rafiki zangu, swala kuu hapa ni nini haswa? Mbona inaelekea kwamba adha zote hizo zinavumilika! Ukizingatia UKIMWI ni soo!

Kwa maoni yangu naamini kwamba kuna mchanganyiko wa hisia za kisaikolojia na pia ugeni wa kifaa chenyewe. Kama haujawahi kubadilisha tube ya tairi, sio rahisi kuziba slow puncture mwenyewe!

Kitu cha kwanza ni kutoa uoga wa kununua bidhaa yenyewe, acha kununua uchochoroni au kwa mshikaji, ingia pharmacy ambapo unahakika watakua wamezitunza vizuri.



Pili, kondomu zipo za aina nyingi sana! Zipo zenye utofauti wa rangi(nyingine hung'aa kwenye giza), zipo za ladha na unene tofauti. Kondomu zina nakshi kibao. Zipo zenye mpira mwembambaaaa, mpira mnene, za ngozi ya wanyama, zipo zilizowekewa ukakasi wa mint, zipo zenye ladha ya matunda na pipi, zenye vijinundu nk. Kuwa mtaalamu wa zote, siri hapa ni kuzijaribisha.

Pia, kuna kondomu za kike!

Tatu ni kumshirikisha mwenzako katika kukifahamu kifaa. Tendo la kutumia kondomu halinogi bila mwenzako kuelewa unajisikiaje ama wewe kufahamu kama mwenzako anaipatapata! Kurahisisha mchezo, ni vema mnunue nyingi, kisha kila mara mchague aina ambayo mtaisikilizia. Mchezo huu utasababisha mrelax na mshiriki tendo kwa akili moja.


Nne, ufundi ni jambo la msingi katika tendo, inashauriwa kwamba mpenzi wako wa kike akuvalishe kondomu. Hii inakupa wewe mwanaume nafasi ya kuendelea kuhamasika kwa kushikwashikwa au kuendelea kumpagawisha mwenzako wakati anakuvisha. Pia, inampa mwenzako nafasi ya kukuona vizuri (kukagua usafi na afya pia!) na kukurusha roho zaidi.


Tano, ukitumia kondomu mara kwa mara, nahakika akili yako itasababisha hisia zizoee na hatimaye utaweza kutenda tendo kama vile unalifanya bila mpira! Mpenzi wako naye atajua ni jinsi gani akuridhishe. Hivyo wote mtafurahia tendo lenu.


Kumbuka, ni utundu na ubunifu. Pila ni kushinda hisia zako na kutumia kifaa kondomu kwa usalama wenu. Wanawake wengi wanasema wapo tayari kusamehe makosa ya wanaume wao wanaotembea nje kama wameonyesha angalau akili ya kutumia kinga! Hakuna mtu anayetaka kuletewa maradhi!

Pombe na madawa ya kulevya vinapunguza kwa kiwango kikubwa matumizi sahihi ya kondomu!








Poa! Nimesema yangu, nakaribisha maoni yenu!

No comments:

Post a Comment