Saturday, July 17, 2010

SOMA UJUMBE UUPATAPO!!!

Mgonjwa mmoja mahututi alikuwa
hawezi kuongea, alipofikishwa hospitalini akawekewa oxgen.
Bac mchungaji akaja kumuombea.
WAKATI AKIOMBEWA, yule mgonjwa
akachukua kalamu na karatasi,
Akaandika haraka haraka na akampa yule Mchungaji. Ambaye
badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye
mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi
yule mgonjwa, AKAKATA ROHO.
Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua
ni wosia wa marehemu. Akasubiri baada ya
mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema;
"KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU
NILIYOKUA NAMUOMBEA"
Akampa mmoja wa wanandugu akisome.
Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na
yule mgonjwa:
"UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN,
NAKOSA HEWA"

No comments:

Post a Comment