WEWE NI MPENZI WA MAGARI NA MDAU WA KARIBU??
Mambo vipi mdau?
Tazama hiyo attached flyer, it says it all.
Ila kwa kifupi tuh ni kwamba kuna tamasha la magari a.k.a Car Show ya
pili, ya kwanza tuliifanya mwaka jana pale Leaders, ya mwaka huu
tunafanyia pale TTCL Kijitonyama, ilipofanyikia show ya Beenie Man,
kutakuwa na maonesho ya magari makali bongo, talk of X6, Ferrari, Bentley,
Lamborghini, Hummer H3,Porsche Carrera, you name them,huamini kwamba yapo
bongo??Njoo uyaone basiiii, watoto wa Bakhresa wanaleta fleet yao yote
uwanjani,nadhani wanajulikana kwenye ishu ya magari yenye adabu hapa mjini
sihitaji kuongelea hilo sana,na kwa upande wapili kuna wadosi wabishi nao
wanaleta vitu vya kujibu mapigo so itakuwa kama mashindano flani ya nani
ana kitu kikali zaidi mjini,famous car yards in town pia wanaleta gari zao
siku hiyo, talk of Tokyo Cars, talk of Samoyaz, Car Mart na wengine wengi,
pia kutakuwa na The Most Pimped Cars in town, gari zenye muziki babu kubwa
zaidi kuliko yote, classic cars za 1940's,kutakuwa na maonesho ya misele
ya hatari,magari yatauzwa siku hiyo uwanjani pale pale,mapya,ya
zamani,hata kama una gari unaliuza pale unakuja nalo unakutana na possible
wateja mbali mbali,pia kama unataka kununua gari basi njoo pale uwanjani
ukutane na vyombo mbali mbali kwa ajili yako.Njoo uone magari uliyozoea
kuyaona kwenye video za kina 50 Cent,njo uyasogelee,uyaguse,upande,na
upige nayo picha vile uwezavyo.
Njoo ukutane na wataalamu wa kupamba magari, wauzaji wa vifaa vya kupambia
magari, wataalamu wa ku-pimp magari, hata kama unataka new body kit ya
gari lako liwe kama la star fulani,njoo utakutana na wataalamu siku hiyo
wakupe ushauri wa namna ya kulipimp gari lako, si unajua mambo ya "Pimp my
ride" ile ya Exzibit kwenye MTV???Basi njoo uonane na wataalamu wa maswala
yale hapa bongo.Wataalamu wa mifumo ya ulinzi wa magari pia watakuwepo.
Kama unahisi una gari kali, au iliyopimpiwa kisawasawa unaruhusiwa kuja
kushowcase it.Kwa ambaye atakuja na mkoko kwa ajili ya kuonesha wadau
kiingilio kitakuwa bure!Tunakaribisha pia ma-star wa bongo kuja na wao na
mikoko yao kutuonesha utofauti wa kuwa mtu wa kawaida na kuwa celebrity.
Apart from that kutakuwa na nyama choma as usual,bata kwa sana,live
performances,kids zone so unaweza kuja hata na mtoto/watoto maana kutakuwa
na michezo ya watoto pia, a kind of a family day out event.
Come show your support, ni kuanzia tarehe 2 - 4 Octber 2009, muda ni saa
tatu asubuhi hadi saa 12 jioni kwa siku zote tatu.Kiingilio ni elfu 2 tuh
kwa kila kichwa.Tuma ujumbe huu kwa watu wako ili uwaambie na wengine
tafadhali, hii si ya kukosa.KARIBU SANAAAA!!!
Kumbuka hili ni tamasha la kila mwaka.
Kwa maelezo zaidi tembelea www.autofest.co.tz
Rgds,
MLAY, Evans Eddy
Tech Director
Tanzania Automotive Festival (Autofest)
P.O. Box 79896
Dar es Salaam, Tanzania.EA
Email: info@autofest.co.tz
Phone: +255 22 2664283
Fax: +255 22 2771265
Hotline: +255 715 847 466 / +255 717 330 817
Website: www.autofest.co.tz
Blog: http://tanzaniaautofest.
No comments:
Post a Comment